Jinsi ya kujiunga na shule yetu
Fomu ya maombi inapatikana katika ofisi ya shule Mafinga kwa gharama ya TSh 25,000/=
Pia unaweza kupakua fomu hiyo kwenye mtandao wetu huu kwa gharama ya TSh 30,000/=
Tafadhali bonyeza hapa kusoma maelezo ya kina kabla ya kulipia fomu
Maelekezo ya kununua fomu mtandaoni
- Lipia TSh 30,000/= kwenye mojawapo ya namba zifuatazo
 |
0673 779 102 Jina: BETHEL SECONDARY |
 |
0743 355 344 Jina: BETHEL MAFINGA |
Tumia namba ya simu kufanya malipo. Usiweke pesa kwa wakala wala kuhamisha toka benki kuja kwetu moja kwa moja.
Ukitumia wakala / benki hatutapata namba ya simu iliyofanya malipo hivyo mifumo yetu haitaweza kushughulikia muamala wako
-
Ndani ya muda mfupi tutakutumia ujumbe kwenye namba uliyoitumia kufanya malipo. Ujumbe huo utakuwa na token.
-
Bonyeza Pakua fomu. Ingiza namba ya simu uliyotumia kufanya malipo.
-
Ingiza token tuliyokutumia kwa ujumbe mfupi
-
Ingiza majina mawili ya mwanafunzi kwenye sehemu husika, kama alivyosajiliwa kwenye mtihani wa darasa la saba.
-
Chagua lugha atakayoitumia mwanafunzi kufanya mtihani wa kuingia.
Iwapo mwanafunzi amemaliza darasa la saba kwenye shule ya English Medium chagua English.
La sivyo chagua Kiswahili.
-
Hakiki jina la mwanafunzi na lugha. Hutaweza kubadilisha baada ya hatua hii.
Kama ni sawa bonyeza Hifadhi Taarifa
-
Pakua fomu. Ichape na ufuate maelekezo yake.
-
Urudi na fomu ya maombi na vyeti vya mwanafunzi siku ya mtihani, Jumatano tarehe 16 September 2026, shuleni Mafinga.
Kwa msaada piga namba zifuatazo: